Ukurasa huu utaelezea sehemu muhimu za mchanganuo wa biashara kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati. Mchanganuo wa biashara ni maelezo ya kina ambayo inaonyesha biashara yako ilikotoka, inakokwenda, hali ya masoko, sekta, kifedha na uongozi wa biashara yako. Ni taarifa muhimu ya kuwavutia watoa mikopo kama benki na taasisi za fedha, wawekezaji na viongozi wa kampuni/shirika
I.
Kasha la nje: Sehemu ya kichwa cha mchanganuo wa biashara.
Anuani ya kampuni
Anuani ya maofisa
Tarehe ya kuandika mchanganuo.
Anuani ya mtayarishaji/watayarishaji
Namba ya toleo la mchanganuo
II.
WAZO LA BIASHARA (AU MUHSTASARI)
Hii ni sehemu muhimu ya kueleza kusudio au wazo la biashara yako kwa muhstasari. Mambo mhimu hapa ni:
Kampuni/biashara itakuwa na ofisi zake wapi?, lini itaanza?, wasifu wa nani kaandika, unauza au kuzalisha nini?, soko lako ni lipi?, utawafikiaje wateja?, na makisio ya bajeti, mauzo, gharama na faida (ambatanisha na chati na au jedwali
Nani ataongoza na uwezo wao
Malengo ni yepi na ni kwa nini unafikiri biashara itafanikiwa
Kama utahitaji mtaji kutokwa benki, wawekezaji au wenye hisa ni kwanini, kiasi gani?, utalipaje? na faida kwa wenye hisa, wawekezaji au benki
Kumb: Usiandike wazo la biashara kabla hujamaliza kuandika mchanganuo wako kwani ni muhstasari wa mchanganuo wenyewe
III.
YALIYOMO (Orodhesha sehemu muhimu tu katika mchanganuo wako) IV.
SEHEMU YA I: MPANGILIO WA BIASHARA
Kuna nini hapa?
Sehemu hii iwe na muhstasari wa biashara na utawala au wahusika katika kusimamia biashara,yaani mameneja na watumishi wengine
A. MUHSTASARI WA BIASHARA
Kwa ufupi eleza ni asili au mrengo au sekta gani biashara yako inaangukia, lini na kwa nini ilianzishwa. Pia eleza yafuatayo:
Maono
Wito
Eleza filosofia ya biashara yako na kwanini unafikiri ni tofauti na zingine. Yaani biashara yako itakuwaje ya kipekee
Mkakati (eleza mikakati uliyonayo kufanikisha biashara yako)
Mikakati yako inahusianaje?
Uchambuzi wa mazingira ya biashara (eleza nguvu na fursa ambazo zitawezesha biashara ifanikiwe. Pia eleza madhaifu na hatari zitakazokwamisha biashara) ni vizuri pia ueleze utazimuduje au kuzikwepa ili biashara isife
B. MAELEZA JUU YA BIDHAA AU HUDUMA
Kama wewe unazalisha au ni muuzaji wa jumla, fafanua juu ya bidhaa zako, eleza kwa ufupi juu ya hatua za kuzalisha, jumuisha taarifa ya kampuni zinazokupa huduma pamoja na upatikanaji wa bidhaa na malighafi pamoja na mambo ya stoo.
Kama biashara yako ni ya uchuuzi: fafanua juu ya bidhaa zako, taarifa ya kampuni zinazokupa huduma pamoja na upatikanaji wa bidhaa pamoja na stoo.
Kama biashara yako ni ya kutoa huduma: orodhesha huduma za biashara
C. HATIMILIKI
Elezea juu ya hatimiliki ya kazi zako, nembo za biashara na uhalali wa kumiliki kazi za wengine (Copyrights, Trademarks, and patent)
Ushahidi wa kusajili, picha na nk (Back up in Supporting Documents with registrations, photos, diagrams, etc )
E. MFUMO WA KISHERIA BIASHARA YAKO
Elezea mfumo wa biashara yako na kwa nini umechagua iwe hivyo
Orodhesha wamiliki wa kampuni husika
F. UONGOZI
Orodhesha watu watakaoendesha biashara yako
Fafanua kazi zao
Toa makadirio ya mishahara
Ambatanisha wasifu na taarifa zingine muhimu
G. WAFANYAKAZI
Utakuwa na wafanyakazi wangapi katikk kila idara?
Je ni sifa zipi zinatakiwa?
Elezea juu ya mishahara
Elezea mahitaji ya baadaye ya wafanyakazi
H. MASUALA YA FEDHA
Nani atahusika wapi kama vile mfumo utakaotumika, tehcnolojia, na idara nyeti za uhasibu
I. MASUALA YA SHERIA
Nani atakuwa mwanasheria wa kampuni au masuala ya sheria yatafanywaje?
I. MASUALA YA BIMA
Bima zipi zitawekewa bima na kampuni na kwa nini?
J. USALAMA
Elezea jinsi gani vifaa vua stoo, ofisi na pesa zitalindwa
SEHEMU YA II: MPANGO WA MASOKO
Elezea juu ya mpango wa masoko na mgawanyiko wake na jinsi biashara yako itakavyoweza kushindana na kumudu ushindani wa kibiashara
Elezea yafuatayo
Uchambuzi wa masoko
Walengwa
Washindani wako (Elezea juu ya uwezo wao na udhaifu wao)
Mwelekeo wa soko
Utafiti wa masoko ( njia, uchanganuzi wa takwimu, na utoaji wa matokeo)
C. MKAKATI WA MASOKO
Bajeti itakuwaje ya masoko
Mbinu za kuuza na kuwafikia wateja
Usindikaji
Mfumo na Sera ya bei ya ushindani
Utambulisho wa biashara yako
Utunzaji takwimu za masoko
Mkakati wa kuuza kama vile kwa kutumia barua pepe, maajenti, nk
Mkakati wa kutoa motisha na promosheni katika mauzo
Mkakati wa kutangaza kama kupitia website, magazeti, TV, au NENO la MDOMONI
Mkakati wa mahusiano na wateja kama vile kushiriki kwenye tamasha mabalimbali nk
Kujisajili katika mitandao mbalimbali nk
D. HUDUMA KWA WATEJA
Kazi gani utafanya kuimarisha huduma kwa wateja?
Elezea malengo ya kufikia ubora wa kutoa huduma
E. UTEKELEZAJI WA MASOKO
Utendaji wa ndani
Kuwatumia wataalamu wa nje
VI.
SEHEMU YA III: TAARIFA YA FEDHA
Elezea maeneo muhimu ya fedha itakayohusika katika sehemu hii
A. Muhtasari wa mahitaji ya fedha
Elezea kwanini unahitaji pesa?
Unahitaji kiasi gani?
B. MAELEZO YA MIKOPO
Ni lazima
(1) Ueleze ni jinsi gani utautumia huo mkopo ukipewa (2) Ambatanisha na taarifa muhimu kama risiti, mikataba nk
C. MAKISIO YA MZUNGUKO WA FEDHA (CASH FLOW FORECAST)
Hii ni ripoti muhimu ambayo huonyesha kama biashara yako itakuwa na uhai au la katika kipindi cha miaka 3 mpaka 5 ijayo
D. MAKISIO YA MAPATO KWA MIAKA 3 HADI 5
Kisia juu ya mapato na matumizi na faida ghafi itakayopatikana kwa miaka 3 hadi 5
E. TAARIFA MAKISIO YA DHAMANI YA BIASHARA YAKO (PROJECTED BALANCE SHEET )
Kisia mali, madeni na dhamani halisi ya kampuni yako ktk kipindi cha miaka 3 hadi 5
F. UCHANGANUSI WA KUFIKIA MAUZO
Elezea ni kiasi gani cha mauzo kwa mwezi itawezesha kampuni yako kurudisha gharama
G. TAARIFA YA FAIDA NA HASARA (PROFIT & LOSS STATEMENT)
Kisia juu ya mapato na matumizi na faida na hasara itakayopatikana kwa miaka 3 hadi 5
H. MAHSABU YA UWIANO WA SEHEMU MUHIMU ZA BIASHARA (BUSINESS RATIOS)
Elezea uwiano kati ya bidhaa za stoo na mauzo, kati ya gharama za kununua bidhaa na mauzo, kati ya mishahara na mauzo nk
[...] Mchanganuo wa biashara ni maelezo ya kina ambayo inaonyesha biashara yako ilikotoka, inakokwenda, hali ya masoko, sekta, kifedha na uongozi wa biahara yako. Ni taarifa muhimu ya kuwavutia wawekezaji na watoa mikopo kama mabenki [...]
[...] Mchanganuo wa biashara ni maelezo ya kina ambayo inaonyesha biashara yako ilikotoka, inakokwenda, hali ya masoko, sekta, kifedha na uongozi wa biahara yako. Ni taarifa muhimu ya kuwavutia wawekezaji na watoa mikopo kama mabenki [...]