Njia 7 za kupata mtaji wa biashara - kivuyo

Sehemu ya III: Njia za Kupata Mtaji wa Biashara

  1. Mali Binafsi

Kama una shamba, fedha, nyumba, gari, mifugo, mazao nk unaweza kutumia mali hizi kama mtaji wa biashara

  1. Wabia wa Biashara

Saa nyingine unatakiwa kuwatumia watu wengine ili kupata yafuatayo

  1. Mtaji wa mali
  2. Mtaji wa mawazo na fikra tofauti
  1. Wawekezaji wa Biashara

Wawekezaji ni watu ambao wanaweza toa mali na pesa zao kukuwezesha wewe kufanya biashara yako lakini wao watahitaji baada ya muda wa uwekezaji warudishiwe pesa au mali zao na riba mliokubaliana kwenye mktaba wa uwekezaji.

  1. Mkopo Kutoka kwa Watu wa Karibu

Ndugu/jamaa/marafiki na majirani wanaweza kuwa ni chanzo kizuri ya mtaji usio nariba.

Wanaweza kukupa fedha taslimu, wanyama, vitu kama mashine, mitambo, nyumba, ardhi, gari, kompyuta, na vifaa mbalimbali

  1. Mkopo Kutoka Kwenye Vyama, Vikundi nk

Vyama vya kijamii, kitaaluma, vikundi vya kuweka na kukopa, Vikoba vinaweza kuwa chanzo cha karibu kupata mkopo wa biashara wenye riba na masharti nafuu. Unachotakiwa tu ni kuwa mwanachama wa chama chenye kukopesha na kufuata masharti ya chama husika.

  1. Mkopo Kutoka Kwenye Mashirika ya fedha (Micro-Credit Enterprises)

Mashirika kama Pride Tanzania, Vision Tanzania (zamani ikiitwa SEDA), Finca, Faida nk ni hatua nzuri kwa biashara ndogo kwani nao kama ilivyo vikoba wanatoa mikopo midogo kwa masharti nafuu.

  1. Mkopo kutoka Benki na Tasisi kubwa za Fedha

Mkopo unaohusisha benki ni sharti iwe ni biashara kubwa na mhusika awe na uhakika na soko pamoja na mtaji kurudi.

Mabenki mengine wanatoa mikopo mikubwa na midogo kwa pamoja.

Soma zaidi Njia 7 za kupata mtaji wa biashara

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi