Uandishi wa MemArt- Memorandum and Articles of Association

Jinsi ya kuandika Memart (Memorundum and Article of Association)

Utangulizi Kuhusu MEMART

MemArt ni kifupi cha Memorandum and Article of Association. Hii ni mkusanyiko wa taarifa za kisheria na za kitaasisi ambazo zote kwa pamoja zinatoa mwongozo wa namna kazi za kampuni zifanyike na mgawanyo wa hisa kwa majina

Memorandum of Association: hii taarifa inaelezea zaidi jina la kampuni litaitwaje, ofisi zake zitakuwa wapi, kazi za kampuni zitakuwa zipi, ukubwa wa hisa, mgawanyo na dhamani  ya hisa, wenye hisa kwa majina yao na hisa zao pamoja na sahihi zao. Pia mwishoni kuna sahihi na mhuri wa mwanasheria wa uma kama anayedhibitisha hiyo taarifa.

Article of Association: hii taarifa inaelezea zaidi uwajibikaji wa kisheria kwa uendeshaji mzima wa kampuni kuanzia masuala ya hisa kisheria, mikutanoupitishwaji wa maazimio, upigaji kura, wakurugenzi wa kwanza wa kampuni, majukumu ya wakurugenzi kisheria, mkutano wa wakurugenzi, kukosa sifa za kuwa mkurugenzi, maswala ya kugawa faida kwa wenye hisa, masuala ya fedha na ukaguzi wa mahesabu, matangazo, kufanyia marekebisho article.  Pia mwishoni kuna sahihi na mhuri wa mwanasheria wa uma kama anayedhibitisha hiyo taarifa.

MEMART ina sehemu kuu tatu (3)

  1. Kasha la nje
  2. Memorandum of Association
  3. Articles of Association

Kasha la nje

Hii ni sehemu ya nje kabisa ya taarifa yako, kama MemArt ni kitabu, basi hii itakuwa ni fron cover ya kitabu chako.

Katika sehemu hii tunaweka zaidi kichwa cha taarifa nzima ukinukuu sheria ya makampuni ya mwaka 202. Sehemu hii pia inatakiwa kutaja kama kampuni ni ya binafsi au ya uma, ni ya hisa au ya udhamini nk.

Mwisho lakini sio mwisho kabisa sehemu hii inatakiwa itaje pia vichwa vya taarifa zote mbili yaani Memorandum of Association na Articles of Association.

Halafu mwisho kabisa kasha la nje litaje nani ameandaa hiyo MemArt na anuani yake. Muandaaji awe ni kati ya wenye hisa

Memorandum of Association

Hii ni sehemu ya pili kabisa ya MEMART ambayo ina sehemu kuu tisa:

  1. Kichwa cha taarifa
  2. Jina la kampuni
  3. Ofisi ya kampuni
  4. Kazi za kampuni (ziendane na mfumo wa ISIC -International Standard Industrial Classification)
  5. Tamko la usalama wa wanahisa
  6. Maelezo ya hisa za kampuni kuanzia idadi za hisa, mgawanyo wa hisa na dhamani ya kila hisa. Maelezo ya mabadiliko yeyeote kwenye hisa
  7. Tamko la kukubali kununua hisa za kampuni
  8. Majina, anuani, idadi ya hisa na sahihi za wanahisa
  9. Sahihi ya mwanasheria na muhuri wake kama shahidi

Articles of Association

Hii ni sehemu kuu ya pili ya MEMART ambayo kwa ukweli inatafsiri tu sheria ya Makampuni ya Mwaka 2002 na maboresho yake kama ilivyotolewa kwa miaka tofauti. Inashauriwa kumtumia mwanasheria aliyebobea kwenye haya mambo ya kisheria kwa upande wa makampuni ili akusaidie vizuri namna ya kuiweka sehemu hii

Pamoja na mambo mengi ya kisheria sehemu hii pia inatoa fursa ya kuorodhesha wakurugenzi wa kwanza wa kampuni, majina, anuani, idadi ya hisa na sahihi za wanahisa pamoja na sahihi ya mwanasheria na muhuri wake kama shahidi

Sehemu muhimu kwenye article of association ni:

  1. Kichwa cha taarifa
  2. Tafsiri na ufafanuzi
  3. Masuala ya hisa
  4. Mabadiliko ya mtaji
  5. Mkutano mkuu wa wanahisa
  6. Wito wa mkutano wa wanahisa
  7. Dondoo za mkutano wa wanahisa
  8. Kura za wanahisa
  9. Wakurugenzi wa kwanza
  10. Nguvu na kazi za wakurugenzi
  11. Maazimio bila kukutana
  12. Mhuri wa kampuni
  13. Kukosa sifa za kuwa mkurugenzi
  14. Mzunguko wa wakurugenzi
  15. Dondoo za mkutano wa wakurugenzi
  16. Usimamizi wa kampuni
  17. Mgawo wa faida na hifadhi ya mtaji
  18. Masuala ya mahesabu ya kampuni
  19. Masuala ya ukaguzi wa mahesabu ya kampuni
  20. Matangazo mbalimbali
  21. Ukumbusho
  22. Mabadiliko ya article
  23. Usalama wa fedha za kampuni
  24. Majina, anuani, idadi ya hisa na sahihi za wanahisa
  25. Sahihi ya mwanasheria na muhuri wake kama shahidi

Hitimisho

Uandishi wa MemArt unatakiwa uende sambamba na usajili wa kampuni. Mwanasheria anayekuthibitishia memart kwa kusaini anatakiwa awe tayari kutoa huduma hiyo tena kwa sababu kuna uwezekano mkubwa memart ikarudiwa kusainiwa kwa sababu BRELA wanaweza kukukatalia jina la awali.

Hii unaweza kuepuka tu endapo utaanza usajili kwa kuhifadhi jina kupitia website ya BRELA kabla ya kulisajili (Company Name reservation). Hifadhi ya jina ni Shs 50,000 kwa siku 60.

Kwa wale ambao kwa sababu moja au nyingine hawataweza kuandika MemArt na au kusajili kampuni, ninatoa huduma hii kwa gharama nafuu kabisa na kwa haraka.

Kwa kuwajali watembeleaji na wafuasi wa tovuti ya KIVUYO>COM, nimeweka “Hatua 10 rahisi kabisa za kusajili kampuni yako kupitia mtandao wa BRELA“. Kama pamoja na taratibu hizo unaona bado unahitaji ushauri na au huduma kamili ya kusajili kampuni, wote mnakaribishwa kwa huduma nzuri, rahisi na ya haraka kwa gharama nafuu.

Kwa maelezo zaidi kuhusu gharama za usajili bofya hapa

  1. Gharama za Kusajili Jina la Biashara BRELAKusajili jina la biashara
  2. Kusajili wa kampuni isiyo na hisa
  3. Kusajili wa kampuni ndogo ya chini hisa za Shs milioni 1
  4. Kusajili wa kampuni ya kati hisa za Shs milioni 1 hadi milioni 5
  5. Kusajili wa kampuni ya kati hisa za Shs milioni 5 hadi milioni 20
  6. Kusajili wa kampuni ya kati hisa za Shs milioni 20 hadi milioni 50
  7. Kusajili wa kampuni ya kati hisa za zaidi ya Shs milioni 50

Gharama za usajili wa kampuni BRELA kwa ufupi ni

Hatua saba (7) muhimu za kufuata wakati wa kufanya usajili wa kampuni au jina la biashara

  1. Kulipia angalau 60% ya malipo yote, Kutuma taarifa zinazotakiwa (taarifa za kampuni, wenye hisa, wakurugenzi, katibu, hisa nk) – siku ya kwanza
  2. Utengenezaji wa nyaraka muhimu za usajili, utiaji saini na kupigwa muhuri wa mwanasheria – siku ya pili
  3. Kuanza mchakato wa maombi masafa na kupakia taarifa kwenye mtandao  – siku ya tatu
  4. Kufanya malipo ya usajili BRELA na kutuma maombi – siku ya tatu
  5. BRELA kuyafanyia kazi maombi kwa kuhakiki na kutoa mapendekezo kama yapo – siku ya nne, saa nyingine hapa huchukua siku nyingi zaidi hadi 3 au zaidi ya hapo
  6. Kuyafanyia kazi mapendekezo ya BRELA kama yapo kama hayapo ndio mwisho.  Kama marekebisho yapo, mchakato unarudi pale marekebisho yalipofanyikia. mfano kama marekebisho yamefanyikia hatua ya kwanza, mchakato wote unaanzia hapo nk – siku ya tano
  7. Kumalizia malipo 40% na kukabidhiwa vyeti na MemArt katika mfumo wa PDF

Kumb:

  1. Mchakato wote huchukua siku tano (5) kama BRELA hawakupendekeza marekebisho
  2. Siku za mchakato zinaweza kupungua kutoka siku tano (5) hadi siku tatu (3) kama taarifa zilizoletwa na mteja ni sahihi, zinajitosheleza na zimeletwa kwa kuwahi.
  3. Ikiwa BRELA watarudisha marekebisho ya jina au taarifa zingine, mzunguko wa mchakato utarudi na kuanzia pale marekebisho yamefanyika. mfano kama marekebisho ni ya jina basi mchakato utarudi na kuanzia kwenye hatua ya kwanza japo utekelezaji wake utaenda kwa haraka zaidi kwa sababu ni marekebisho tu. Kama marekebisho ni ya ujazaji wa fomu za BRELA tu basi mchakato utarudi kwenye hatua ya tatu nk.
  4. Mteja atalazimika kupendekeza majina ya kipekee (Unique names) matatu (3) kwa ajili ya usajili na jina la kwanza likibeba uzito zaidi ya jina la pili na kadhalika jina la pili likibeba uzito zaidi ya jina la tatu.
  5. Idadi ya marekebisho ya jina inayoruhusiwa kwa ada ile ile ni matatu tu, zaidi yahapo mteja atawajibika kulipa Shilingi elfu ishirini (Shs. 20,000) kwa kila jina linaloongezeka.

MZUNGUKO WA MCHAKATO WA KUSAJILI KAMPUNI BRELA

Maelezo zaidi ya namna ya kusajili biashara au kampuni BRELA

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi