Ulicho Nacho Mkononi ni Mtaji Tosha wa Biashara

“BWANA akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo.” 

Kutoka 4:2

Hakika ulichonacho MKONONI inatosha kabisa kubadili maisha yako

Musa alishika fimbo tu hakuwa na kitu kingine

Wewe unaweza kuwa na afya nzuri, familia nzuri, eneo unaloishi ni zuri, kipawa chako ndiyo fimbo yako ambayo Mungu anaweza itumia kuikombolea Israeli.

Waswahili walisema “Fimbo ya mbali haiuwi nyoka” mimi nakubaliana na usemi huu kabisa

Vitu ambavyo huna, na ambazo ziko mbali na wewe kamwe haziwezi kabisa kuyabadilisha maisha yako ya kimwili na au ya kiroho.  Shika sana ulicho nacho mwovu asije akakunyang’anya

Sikiliza hadithi hii

“Mtu mmoja baada ya kutafuta kazi sana mpaka soli zote za viatu vikaisha na yeye baada ya kujichunguza akajikuta mkononi ana Shs 10,000/= tu.

Kwa hasira alijiuliza sasa kazi zote nimetafuta na nimekosa, ngoja tu nikauze vitunguu an nyanya

Jamaa alikwenda sokoni kununua Vitunguu na nyanya vya Shs. 10,000 na kuanza kuvitembeza kwa majirani. Yaani jamaa alianza kazi ya umachinga wa bidhaa za vyakula na majumbani.

Baada ya kumaliza raundi ya kwanza, ile Shs 10,000 ikazaa 10,000 nyingine. Akaenda tena sokoni kununua Vitunguu vya 20,000 akatembeza kwenye nyumba zingine na kupata faida ya Shs. 20,000. Kwa siku hiyo alifanikiwa kuzungusha roundi nne na jioni wakati anahesabu akajikuta alikuwa na zaidi ya Shs. 80,000.

Jamaa alijisema

“Kumbe umachinga unalipa”

Akaadhimia kutoendelea tena na zoezi lake la kutafuta kazi badala yake atakuwa mmachinga wa kuuza vyakula na bidhaa za majumbani.

Jamaa aliendelea kufanya vizuri kwani ndani ya miaka mitatu akawa ana pickup yake ya kusambazia bidhaa hizo

Ilipotimu miaka mitano jamaa sasa anatumia kenta.

Je akifikisha miaka 10 au 15 atakuwa na mtaji wa kiasi gani huyo machinga?

Ulichonacho mkononi ndio mtaji wa biashara. Acha kuwasumbua benki kwani watakukatisha tamaa

Acha kuwasumbua ndugu na marafiki nao watakukatisha tamaa

Jiangalie mkononi una nini?

  1. Je una kipawa
  2. Inaweza kuwa ni mzungumzaji mzuri?
  3. Mwimbaji mzuri?
  4. Mchoraji mzuri?
  5. Mkimbiaji sana?
  6. Mwogeleaji sana?
  7. Kucheza mpira?
  8. Kushawishi wengine?
  9. We ni mrefu sana?
  10. We ni mbilikimo?
  11. Una pua ndefu hadi futi mbili?
  12. Eneo unaloishi ina fursa nyingi sana?
  13. Uko karibu na mto, ziwa ,mlima, mbuga za wanyama, mawe, udongo wa ujenzi, mchanga, mimea mizuri nk

Yawezekana ulichonacho mkononi ni zaidi ya hayo hapo juu, changamka sasa na uhatamie hizo fursa ili kuyabadili maisha yako.

Mwalimu JK Nyerere aliwahi kusema kuwa

“Linalowezekana leo lisingoje kesho”

Hebu FUNGUKA sasa

Angalia mkononi mwako kuna nini?

Weka mikakati ya kutumia ulichonacho mkononi na Mungu atakusaidia ujikomboe sana

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi